Tafuta kitu cha kufanya katika maisha yako unachokiamini zaidi kuliko pesa, kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika kwa mfano, na ukishakipata kuwa kiongozi na mkarimu kwa wengine. Kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika inaweza kuwa ndiyo nafasi yako uliyopangiwa na Mungu uitumie kwa manufaa ya wengine, si kwa manufaa yako, nafasi za wengine zitatumika kwa manufaa yako. Kuna vitu vingi ambavyo mtu anaweza kufanya; chagua kimoja kinacholeta maana zaidi katika maisha yako na ukifanye hicho, kwa nguvu zako zote.

Unapokuwa mbali na Mungu unakuwa mbali na mwanga, unakuwa gizani, unakuwa mbali na joto, unakuwa katika baridi ya milele. Unapokuwa katika baridi ya milele rangi ya ngozi yako itabadilika na kuwa bluu. Macho yako yatakuwa makubwa kama ya nguva. Bluu maana yake ni kuwa mbali na maarifa ya Mungu. Nguva maana yake ni kuwa mbali na utukufu wa Mungu. Kuwa karibu na maarifa ya Mungu na utukufu wa Mungu, usiwe mkristo wa kanisa, usiwe mkristo wa dini, kuwa Mkristo wa Yesu Kristo.

Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako.

1 2