Tafuta kitu cha kufanya katika maisha yako unachokiamini zaidi kuliko pesa, kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika kwa mfano, na ukishakipata kuwa kiongozi na mkarimu kwa wengine. Kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika inaweza kuwa ndiyo nafasi yako uliyopangiwa na Mungu uitumie kwa manufaa ya wengine, si kwa manufaa yako, nafasi za wengine zitatumika kwa manufaa yako. Kuna vitu vingi ambavyo mtu anaweza kufanya; chagua kimoja kinacholeta maana zaidi katika maisha yako na ukifanye hicho, kwa nguvu zako zote.

Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.

Kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa. Wengine wana pesa, wengine wana vipaji, wengine wana muda. Vipaji vyote tulivyopewa na Mungu, vikubwa au vidogo, hatuna budi kuvitumia kiukarimu kwa watu wanaovihitaji. Tunapofanya hivyo tunaleta mabadiliko katika dunia kwa ajili ya watu fulani, na tunapata maana halisi ya maisha na toshelezo la moyo katika maisha yetu.